Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. Katika shamba la ukubwa wa ekari moja (1 acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha tani 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha za kukidhi mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na umasikini.
Kilimo Cha Tiki Ti Maji Pdf 84
Mikoa ya Tanzania: Kilimo cha matikiti maji kinakubali vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.
Angalizo: usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au jioni kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
Magonjwa kama ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea. Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti magonjwa hayo hapo juu.
Asante sana mr. mohammed nimeelewa na nitafanya kadri ya muongozo uliotoa. Lakini naomba kuuliza ni mara ngapi inatakiwa kumwagilia kwa siku tangu ninapokuwa nimepanda mmea.kwa yeyote anaepatikana mkoa wa morogoro,ruvuma,mtwara na lindi na amefanya au anafanya kilimo hiki naomba tuwasiliane kwa simu 0758152710 au 0657152710.Ahsante.
Habari, mimi naomba kuuliza maana nimeshalima matikiti nimekula hasara Ile mbaya, maswal yangu ni 2,.lnasemekana unaweza kulima matikiti mara nne kwa mwaka je unaweza kuniambia ni miez ipi? Swal la pili, wanasema kwamba matikiti yakishakomaa kipindi cha mwisho kama wiki mbili au moja na nusu unayakatia maji ili yaweke sukari, na hili likoje? Naomba kuwasilisha
Pole kwa yaliyokufika.Swali la kwanza: Ukitumia green house, unaweza bila shida. Lakini kwa shamba la wazi ni lazima uepuke maji ya mvua wakati wa maua, lkn pia uhakikishe hakuna maji ya kutuama na mwisho ujidhatiti kudhibiti wadudu na magonjwa ya fungus.
Napimaje ardhi ili kujuwa rutuba kama ina fahaa kwa hicho kilimo cha matikiti..!!? je naweza ku chota udogo wa eneo la shamba nakwenda wanako uza pembejeo na mbegu za mimea wana weza kupima pia..? au sehemu stahiki ni ipi..ili nijirizishe na eneo stahiki..!!?
kilimo cha matikiti katika ukanda wa mto ruvu (mlandizi) kinaweza kukubali bila kuathiri uzalishaji na ubora wa tikiti kama masharti yote ya kilimo hicho yakifwatwa? nikimaanisha hali ya hewa ya eneo inaruhusu?
Labda pia naombeni kuondolewa wasiwasi juu ya kilimo hiki.je jipi kuhusu mkoa wa kagera wilaya ya muleba kilimo hiki ni rafiki wa mazingira?Vipi kuhusu vipimo hivi vya pH,mm za mvua na kiwango cha jotoridi na ubaridi nitavipataje mimi mtu wa hali ya chini kikipato?mbegu na mbolea naweza kuzipata wapi kwa urahisi?vipi kuhusu bei ya vitu hivyo nilivyovitaja?nitashukuru nikipata majibu kupitia email yangu ya [email protected]
Vitu kama mbegu na mbolea vinapatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo ama kwa suala la bei: Urea kwa kawaida ni Tsh 50,000, CAN ni Tsh 55,000 na DAP ni 80,000. Hizo ni bei kulingana na mazingira ya kwetu, hata hivyo bei zinaweza kubadilika kulingana na mazingira kwa hiyo inaweza kupungua au kuongezeka kidogo kwa niliyotaja mimi.
Habari, mimi nimejarib kulima matikiti huko kigambon lkn nilichokipata ni maumivu, nimelaza laki saba nimeambulia laki mbili na nusu. Nimeona hapa muda unaotakiwa lkn mwenyej wangu aliniambia ni miez miwili tu na nilipanda F1ya Kenya. Ila naomba kuuliza coz humu ndani sijakiona, Je ni kweli wiki moja ya mwisho unatakiwa usimwagie ili tunda liweke sukari? Naomba kuwasilisha 2ff7e9595c
Comments